Isaiah 10:1-6

1 aOle wao wawekao sheria zisizo za haki,
kwa wale watoao amri za kuonea,

2 bkuwanyima maskini haki zao
na kuzuilia haki za watu wangu walioonewa,
kuwafanya wajane mawindo yao
na kuwanyang’anya yatima.

3 cMtafanya nini siku ya kutoa hesabu,
wakati maafa yatakapokuja kutoka mbali?
Mtamkimbilia nani awape msaada?
Mtaacha wapi mali zenu?

4 dHakutasalia kitu chochote,
isipokuwa kujikunyata miongoni mwa mateka,
au kuanguka miongoni mwa waliouawa.
Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,
mkono wake bado umeinuliwa juu.

Hukumu Ya Mungu Juu Ya Ashuru


5 e“Ole kwa Ashuru, fimbo ya hasira yangu,
ambaye mkononi mwake ana rungu ya ghadhabu yangu!

6 fNinamtuma dhidi ya taifa lisilomjua Mungu,
ninamtuma dhidi ya taifa linalonikasirisha,
kukamata mateka na kunyakua nyara,
pia kuwakanyaga chini kama matope ya barabarani.
Copyright information for SwhKC